
Vijana wanne wanaenda kukarabati nyumba ya Mba Darti, binti wa Nyai Melati, mwimbaji maarufu wa jadi (sinden). Lakini wanapoanza kazi, matukio ya ajabu na ya kutisha yanaanza kutokea. Wanagundua kwamba Nyai Melati aliuawa kutokana na ushindani wake na sinden mwingine aitwaye Fahma. Majivu ya Fahma yaliyokuwa yamechomwa yanatumiwa na Kliman, aliyekuwa msimamizi wa zamani wa eneo hilo, kujaribu kuwafukuza vijana hao kwa msaada wa Ki Renggo, mtaalamu wa mambo ya kishirikina. Hali inakuwa mbaya zaidi pale roho ya Fahma inapomwingia Darti na kuanza kuwashambulia vijana hao. Mwisho wa yote, Ki Renggo anachoma majivu ya Fahma, jambo linalokatiza nguvu ya roho hiyo na kumaliza haunting iliyokuwa ikiendelea ndani ya nyumba. Kwa kifupi: Ni story ya kisasi, ushindani wa wanamuziki wa jadi, roho ya aliyekufa na nyumba iliyotawaliwa na nguvu za kishetani.
DJ Dax@djdax