
Mwaka 1987, msichana mwenye umri wa miaka 18 akiwa bado katika majonzi baada ya kifo cha dada yake, anaanza kuhisi kwamba familia yake inasumbuliwa na kiumbe cha kutisha. Matukio ya ajabu na ya kutisha yanapoendelea kutokea nyumbani, anaanza kuchunguza chanzo chake. Lakini uchunguzi wake unampeleka kwenye siri nzito na za kutisha zilizofichwa katika historia ya familia yao. Kadiri anavyofichua ukweli, anatambua kwamba kifo cha dada yake na uwepo wa hilo kiumbe huenda vina uhusiano mkubwa kuliko alivyodhani.
DJ Dax